Kuishi kama Yesu

Mungu akasema na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi. —MWANZO 1:26

Katika Mwanzo 1:26, Mungu aliposema, “Na tumfanye mtu kwa mfano wetu…” huu mfano haurejelei kufanana kwa maumbile ya mwili, lakini ya tabia. Tuliumbwa ili tukachukue tabia zake kama zinavyojitokeza ndani ya Mwanawe Yesu.

Lengo kuu la kila aaminiye ni kuwa mfano wa Yesu. Ndiyo wito wetu wa juu kabisa maishani. Ni jambo la kusisimua kujua kwamba tunaweza kukaribiana sana hivyo na Bwana katika uhusiano wetu naye hata tukaanza kukabiliana na hali vile alivyokabiliana nazo yeye na kutendea watu vile alivyowatendea yeye. Lengo letu ni kutaka kufanya mambo vile Yesu angeyafanya.

Yesu ndiye mfano wetu. Katika Yohana 13:15, aliwaambia wanafunzi wake, baada ya kuosha miguu yao kama mtumishi, “Kwa kuwa nimewapa kielelezo; ili kama mimi nilivyowatendea, nanyi mtende vivyo.” Kila siku na kwa kila njia mtazame Yesu na ufuate mfano alioweka katika Neno la Mungu kwa maisha yako ya kila siku.


Mungu atazidi kufanya kazi na kila mmoja wetu kwa neema ili tufike mahali ambapo tutaanza kufanya vile Yesu angefanya katika kila hali ya maisha.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon