Amini katika Nguvu za Mungu

Na Neno langu na kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho  na za nguvu ili imani isiwe katika hekima ya wanadamu, bali katika nguvu za Mungu (1 WAKORINTHO 2:4-5).

Elimu ni muhimu, lakini lazima tukumbuke kwamba hekima ya Mungu ni bora na yenye thamani zaidi kuliko elimu ya ulimwengu na falsafa ya kibinadamu. Mtume Paulo alikuwa mtu mwenye elimu ya juu, lakini akasema kwa ushapavu kwamba ni nguvu za Mungu zilizofanya mahubiri yake kuwa yenye thamani, sio elimu yake.

Ninajua watu wengi ambao wanaofuzu kutoka vyuoni na vyeti shahada ya kwanza na nyinginezo na wana shida ya kupata kazi. Ninajua pia watu ambao hawajakuwa na nafasi ya kwenda chuo ambao humtegemea Mungu kuwapa kibali na wanaishia kuwa na kazi kubwa. Imani yako iko wapi? Iko ndani ya Mungu au katika kile ambacho unajua? Haijalishi tunachojua au tunayemjua, imani yetu inafaa kuwa ndani ya Kristo pekee yake na katika nguvu zake.

Paulo alitaja katika 1 Wakorintho 1:21 kwamba ulimwengu na kila hekima na falsafa yake yote ya kibinadamu ilikosa kumjua Mungu, lakini akachagua kujitambulisha, na kuwaokoa binadamu kupitia kwa upumbavu wa kuhubiri. La kuhuzunisha ni, kila mara tunapata kwamba kadri watu wanavyosoma sana, ndipo inakuwa vigumu kwao kuwa na imani rahisi ya kitoto. Maarifa mengi ya akili na urazini unaweza unaweza kufanya kazi kinyume chetu iwapo hatutakuwa waangalifu, kwa sababu tunaweza kujua Mungu tu kwa Roho na moyo, sio kwa akili zetu. Kuwa na hakika ya kuacha imani yako kutulia katika nguvu za Mungu na sio akili zako ili kukusaidia katika maeneo yote ya maisha.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Nguvu za Mungu zinaweza kushinda vizuizi vyote ambavyo huenda ukakabiliana navyo maishani.  

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon