Amini

Amini

Yesu akajibu, akawaambia, hii ndiyo kazi ya Mungu, mmwamini yeye aliyetumwa na yeye… —Yohana 6:29

Mara nyingi watoto wadogo huamini wanachoambiwa na wazazi wao bila kufikiri, na ndivyo Mungu anavyotaka tuwe naye. Anataka tuamini anavyosema katika Neno lake! Wakristo huitwa “waaminio,” na waaminio wanafaa kuamini!

Je, wewe ni aaminiye anayeamini, au aliyejaa shaka tele? Imani ya kawaida kama ya mtoto huzaa matunda mengi mazuri. Kwa mfano, furaha na amani hupatikana katika kuamini (Warumi 15:13). Shaka, kujiwazia, wasiwasi, na hofu huzaa aina nyingi za mateso, lakini haya yote yanaweza kuepukwa kwa kufanya uamuzi wa kuamini Neno la Mungu. Amini kwamba kitu kizuri kitafanyika kwako. Amini kwamba Mungu anataka kukutana mahitaji yako yote, kwamba anakupenda na anataka kukusaidia wakati wote.

Tunapoamini, basi tunaingia katika raha ya Mungu na kufurahia kabisa kila siku ya maisha yetu. Tunaweza kuishi maisha siku moja kwa wakati na kuamini kwamba mustakabali wetu ni salama ndani ya Mungu.


Ikiwa utashuku chochote, shuku shaka zako!

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon