Anataka Kuhusishwa katika Kila Kitu

Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu hao ndio wana wa Mungu (WARUMI 8:14)

Kuongozwa na Roho Mtakatifu inamaanisha kumruhusu kuhusika katika kila uamuzi tunaofanya, mdogo na mkubwa. Hutuongoza kwa amani na hekima, na pia kwa Neno la Mungu. Huzungumza kwa sauti tulivu ndogo katika mioyo yetu, au kile ambacho mara nyingi tunaita, “ushahidi wa ndani.” Lazima wale wenzetu wanaotamani kuongozwa na Roho Mtakatifu  wajifunze kufuata ushahidi wa ndani na kuitika haraka.

Kwa mfano, ikiwa tunashiriki katika mazungumzo, na kuanza kuhisi kutotulia ndani yetu, huenda akawa ni Roho Mtakatifu akituashiria kwamba tunahitaji kubadilisha mazungumzo yachukue mkondo mwingine au tunyamaze. Tukihisi kukosa utulivu ndani yetu tukiwa karibu kununua kitu, tunafaa kungoja na kupambanua kwa nini hatuna utulivu. Pengine hatuhitaji hicho kitu, au huenda tukapata kiko mnadani mahali fulani, au huenda sio wakati mzuri wa kukinunua. Si lazima kila mara tujue ni nini; tunahitaji tu kutii.

Ninakumbuka wakati mmoja niliokuwa kwenye duka la viatu. Nilikuwa nimechagua aina nyingi za viatu kuvijaribu, mara ghafla nikawa sina utulivu. Ukosefu huu wa utulivu ukaongezeka hadi nikasikia Roho Mtakatifu akisema, “Ondoka dukani humu.” Nikamwambia Dave tuondoke, na tukaondoka kabisa. Sikujua ni kwa nini, na sihitaji kujua. Huenda Mungu aliniokoa kutokana na madhara fulani yaliyokuwa yanakuja, au pengine watu kwenye duka hilo walihusika katika mambo yasiyokuwa ya kimaadili. Huenda yalikuwa majaribu ya utiifu. Kama nilivyosema, si lazima tujue kwa nini Mungu hutuongoza katika njia fulani. Sehemu yetu ni kutii tu sauti yake.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Njia kuu zaidi ya kumheshimu Mungu ni kumtii pasi kusita.  

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon