Anza Ukiwa na Nguvu, Umalize Vyema

Anza Ukiwa na Nguvu, Umalize Vyema

Mkiwezeshwa kwa uwezo wote, kwa kadiri ya nguvu ya utukufu wake, mpate kuwa na saburi ya kila namna na uvumilivu pamoja na furaha. WAKOLOSAI 1:11

Kila kitu tunachofanya maishani kina mwanzo na mwisho. Kwa kawaida huwa tunafurahi mwanzoni mwa jambo, uhusiano, au tukio; tunafurahia tunapoweza kusherehekea mafanikio yetu na kuwa na ridhaa ya matamanio yaliyotimilika. Lakini kati ya mwanzo na mwisho, kila hali ina “katikati”—na katikati ndipo tunapokabiliana na changamoto zetu kuu wakati wote.

Kati ya mianzo na miisho yetu, lazima tudhamirie tuwezavyo kushinda hali ngumu tunazokumbana nazo katikati. Tunaweza kuwa watu wanaomaliza tunachoanza. Na tunaweza kushukuru kuwa si lazima tukifanye peke yetu—Mungu atatusaidia tukimruhusu.

Huenda ukawa katikati ya kitu sasa hivi. Chochote unachojipata katikati yake, muombe Mungu nguvu zake na hekima, na uwe na nidhamu kwa mrefu kidogo, halafu udhamirie kukifanya mpaka umalize.


Sala ya Shukrani

Ninakushukuru, Baba, kwamba siko peke yangu katika hali hii. Uko hapa pamoja nami, na unanipa nguvu ninazohitaji. Kwa usaidizi wako, nimedhamiria kutokata tamaa. Ninaenda kufanya hiki mpaka mwisho na nikupe utukufu kwa mwisho wenye ushindi!

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon