Atakubadilisha

Na roho ya Bwana itakujilia kwa nguvu nawe utatabiri pamoja nao, nawe utageuzwa kuwa mtu mwingine (1SAMWELI 10:6)

Kuweza kusikia sauti ya Mungu ni matokeo muhimu ya kumjua na kujazwa na Roho wake, lakini si kwamba ati huo tu ndio ushahidi wa maisha yaliyojawa na Roho peke yake. Ushahidi mwingine rahisi wa nguvu za Roho Mtakatifu ndani ya mtu ni maisha yaliyobadilika.

Wakati wa mateso ya Yesu, Petro alimkana mara tatu kwa sababu aliwaogopa Wayahudi (soma Luka 22:56- 62); lakini baada ya kujazwa na Roho Mtakatifu katika siku ya Pentekoste, hakuwa na woga tena, lakini alisimama na kuhubiri ujumbe wa kijasiri. Kuhubiri kwa Petro kulipelekea watu elfu tatu kuongezwa kwenye Ufalme wa Mungu siku hiyo (soma Matendo ya Mitume 2:14-41). Ukamilisho wa Roho Mtakatifu ulimbadilisha Petro, ulimgeuza na kuwa mtu tofauti- aliyekuwa mwenye ujasiri, asiye wa kuogopa kabisa.

Siye Petro peke yake aliyechukua msimamo wa kijasiri siku hiyo. Wale wanafunzi wengine kumi na wawili pia walifanya vivyo hivyo. Wote walikuwa wamejifungia na kujificha kwa kuwaogopa Wayahudi Yesu alipowajilia baada ya kufufuka kwake (soma Yohana 20:19-22). Ghafla baada ya kujazwa na Roho Mtakatifu, woga ulitoweka na wakawa wajasiri.

Nguvu za Roho Mtakatifu zimebadilisha watu wasiohesabika kwa kipindi cha miaka mingi. Zilimbadilisha Saulo, vile ilivyorekodiwa katika andiko la leo. Ziliwabadilisha Petro na wanafunzi wengine. Zimenibadilisha; na zinaendelea kuwabadilisha wanaozitafuta ulimwenguni mwote. Je, unahitaji kubadilishwa? Mwombe Roho Mtakatifu akujaze leo.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Unahitaji nguvu za Roho Mtakatifu ili ubadilike.  

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon