Busara

Busara

Mimi, [kutoka kwa Mungu] hekima, nimefanya werevu kuwa kao langu; natafuta maarifa na busara… —Mithali 8:12

Neno ambalo husikii mafunzo mengi kulihusu ni “busara.” Katika Maandiko, “busara” au “kuwa na busara” inamaanisha kuwa wasimamizi wazuri wa vipawa ambavyo Mungu ametupatia kutumia. Vipawa hivyo vinajumlisha uwezo, wakati, nguvu, na afya pamoja na mali zetu. Vinajumlisha miili yetu pamoja na nia na roho zetu.

Mungu amempa kila mmoja wetu vipawa tofauti na neema kulingana na vile anavyotaka tuvitumie. Mtu mmoja anaweza kuwa na kipawa cha kuimba na hufanya hivyo katika eneo dogo analoishi, huku uwezo wa mtu mwingine wa kuimba ukijulikana katika maeneo mengi ya ulimwengu. Biblia inatuambia tutumie vipawa vyetu kulingana na neema tuliyopewa (Warumi 12:6).

Kila mmoja wetu atakuwa na hekima kujua yale tunayoweza kufanya, kuwa na uwezo wa kutambua tunapofikia “kilele” au “kupindukia mipaka.” Badala ya kujisukuma kileleni ili kuwapendeza wengine, kuridhisha matamanio yetu, au kufikia malengo yetu ya kibinafsi, tunaweza kujifunza kumsikiliza Mungu na kumtii. Tukifuata mwongozo wa Bwana, tutafurahia maisha yenye baraka.

Sisi sote hukumbwa na mfadhaiko na wakati mwingine huwa tunahisi athari zake, lakini tujifunze kuudhibiti vizuri. Mwambie Mungu akuonyeshe maeneo katika maisha yako ambayo yanaweza kubadilishwa ili yakusaidie kuondoa mfadhaiko wa ziada kwa njia iliyo bora.


Mungu ni mwema, na anataka ufurahie maisha ya amani tele.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon