Chochea Ukuaji

…Kwa kuwa furaha ya Bwana ni nguvu zenu. —Nehemiah 8:10

Tunapopitia nyakati ngumu, tunaweza kuchukua hatua na kuachilia furaha kabla ya kuanza kupoteza matumaini. Tunaweza kuanza kufurahi hata kama tunajihisi kufanya hivyo au la. Ni kama kuchochea pampu kwa kusogeza kishikio juu na chini hadi isonge ndani na maji yaanze kutiririka.

Ninakumbuka nyanyangu na babu yangu walikuwa na pampu ya kitambo sana. Ninakumbuka nikisimama kwenye beseni la kuosha vyombo nilipokuwa mtoto mdogo, nikisongeza kishikio cha pampu juu na chini na wakati mwingine nikihisi kwamba haitashika vizuri na kutoa maji. Ilihisika kama ambayo haikuunganishwa na kitu chochote, na nilikuwa tu nikivuta hewa.

Lakini nisingekata tamaa, kusongeza kishikio juu na chini ingekuwa kazi ngumu zaidi. Hiyo ndiyo ilikuwa dalili kwamba maji yangeanza kutiririka baada ya muda mfupi.

Hivyo ndivyo ilivyo na furaha. Tuna kisima cha maji ndani ya roho zetu. Kishikio cha pampu cha kuyaleta juu ni uteuzi tunaofanya—kutabasamu, kuimba, kucheka na kadhalika. Mara ya kwanza huenda ishara katika mazingira zisionekane kuwa nzuri. Na baada ya muda mfupi mambo yanakuwa hata magumu, lakini tusipokata tamaa, hivi karibuni tutapata “mlipuko” wa furaha.


Furaha ya Bwana ni nguvu zako. Unaweza kuchagua kuwa na nguvu kwa kuchagua kuishi katika furaha.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon