Chukua Muda Kusikiliza

Chukua Muda Kusikiliza

Bwana, asubuhi asubuhi utaisikia sauti yangu, asubuhi nitakupangia dua yangu na kutazamia. —ZABURI 5:3

Ili kusikia sauti ya Mungu, kuna haja ya kutafuta nyakati ili kutulia tu. Hii ni sehemu muhimu ya kuishi katika uhusiano wa karibu na Mungu. Hivyo ndivyo unavyotambua uongozi wa Mungu katika maisha yako. Mtindo wa maisha yenye shughuli nyingi, pupa, hasira, na mfadhaiko mwingi huwa na changamoto za kumsikia Bwana.

Iwapo una njaa ya kusikia sauti ya Mungu, tafuta mahali na utulie mbele zake. Kuwa peke yako na yeye na umwambie unamhitaji na unataka akufundishe jinsi ya kupokea uongozi na mwelekeo wake. Mwambie akuambie alicho nacho kwa ajili ya maisha yako na kile anataka ufanye siku hiyo.

Halafu ninakuhimiza kufanya hivi: Chukua muda usikize.

Hata kama hutahisi kichocheo katika roho yako mara moja, Mungu anaahidi kwamba ukimtafuta, utampata (Yeremia 29:13). Utapata neno kutoka kwa Mungu. Atakuongoza kwa kujua kwa ndani, kwa hisia ya kawaida, kwa hekima, au kwa amani. Na kila wakati hata kama atakuogoza vipi, uongozi wake utawiana na Neno lake.

Nimepata kujua kwamba Mungu huwa haneni nasi mara moja au wakati tunapoomba. Huenda akaishia kunena nawe baada ya siku mbili ukiwa katikati ya kufanya jambo ambacho hakina uhusiano kabisa. Hata ingawa huenda kisiwe katika wakati wetu, Mungu atanena nasi na kutujuza njia tunayofaa kuchukua.


Kusikiliza ni sehemu muhimu ya wakati wako wa kila siku na Mungu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon