
Basi kwa kuwa Kristo aliteswa katika mwili wake, ninyi nanyi jivikeni silaha ya nia ileile, kwa maana yeye aliyeteswa katika mwili ameachana na dhambi. Tangu sasa msiendelee kuishi katika tamaa za wanadamu, bali katika mapenzi ya Mungu, wakati wenu uliobaki wa kukaa hapa duniani. —1 Petro 4:1–2
Kifungu kizuri cha Petro kinatufundisha siri kuhusu jinsi ya kufaulu katika nyakati na hali ngumu. Hii hapa fasiri yangu ya mistari hiyo:
“Fikiria kuhusu mambo yote ambayo Yesu alipitia na vile alivyovumilia mateso ili kutenda mapenzi ya Mungu, na itakusaidia kufaulu katika hali zako ngumu. Jihami kwa vita; jitayarishe kwa vita kwa kuwaza vile Yesu alivyowaza…”Nitateseka kwa kuvumilia badala ya kukosa kumpendeza Mungu.” Kwa kuwa ukiteseka, huku ukielekeza nia ya Yesu kwa mateso yako, hutaishi tu kujifurahisha, kufanya yaliyo mepesi na kutoroka yote yaliyo magumu. Lakini utaweza kuishi kwa sababu ya, yaliyo mapenzi ya Mungu na siyo kwa hisia na fikra zako za mwili.
Kuna magumu tunayopitia katika maisha, lakini pia huwa tunapitia furaha ya ushindi. Majaribu na mitihani itakuja, na Mungu huitumia kukuza uwezo alioweka ndani yako. Sehemu yako ni kuamua kwamba hutokata tamaa kamwe, kwa vyovyote vile, hadi uone ahadi za Bwana zikitimia katika maisha yako. Kuna mtu mmoja ambaye shetani hawezi kushinda—yule asiyekata tamaa.
Endelea bila kukoma, na utafika.