Fikia Uwezo Wako Mkamilifu

Fikia Uwezo Wako Mkamilifu

Pande zote twadhikika, bali hatusongwi, twaona shaka, bali hatukati tamaa. 2 WAKORINTHO 4:8 BIBLIA

Ninaamini kabisa kuwa kufikia ukamilifu wa uwezo wako kunategemea jinsi unavyokabiliana na matatizo yako. Matatizo si mabaya wakati wote. Kwa kweli, matatizo yanaweza kuwa kitu cha kushukuru kwacho kwa sababu Mungu anaweza kukitumia kukutia nguvu. Winston Churchill alisema: “Kutawala matatizo ni nafasi ya ushindi,” na ninakubali kwa moyo wangu wote.

Ukiruhusu matatizo na changamoto kukufadhaisha, kukutishia, au kukukatisha tamaa, hutawahi kuyashinda. Lakini ukikabiliana nayo ana kwa ana na kukaza mwendo katika matatizo unayopitia, kukataa kukata tamaa katikati ya matatizo hayo na kusonga mbele na moyo wa shukrani, utajenga ujuzi na dhamira inayohitajika na kuwa kila kitu ulichoumbwa kuwa na kuwa na kila kitu ambacho Mungu anakusudia kwa ajili yako.


Sala ya Shukrani

Ninakushukuru, Baba, kwamba silazimiki kukata tamaa ninapokumbana na matatizo—ninaweza kukutana nayo ana kwa ana, nikijua kuwa wewe huwa nami kila wakati. Asante kwa ahadi kuwa Aliye ndani yangu ni mkuu kuliko yule aliye duniani.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon