Furahia Vitu VidogoVidogo

Furahia Vitu VidogoVidogo

Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake ni za milele! 1 MAMBO YA NYAKATI 16:34

Uamuzi unahitajika ili kuanza kufurahia maisha tele tele. Na uamuzi huo huathiri kila kitu—hata maeneo yaliyopuuzwa katika maisha yetu.
Kwa mfano, unaweza kufurahia sio tu kazi yako na mafanikio yako, lakini hata kwenda kazini kila asubuhi. Usifadhaike kuhusu msongamano wa magari na kufikiri utakachofanya ukifika kazini kiasi cha kukosa kufurahia safari hiyo.

Tunaweza kushukuru tukiwa kwenye msongamano wa magari—kushukuru kuwa tuna gari, kushukuru kuwa gari liko katika hali nzuri, kushukuru kuwa tuna kazi, na kushukuru kuwa tuna dakika chache za ziada za kuwa na Mungu huku tukiwa tumekwama katika msongamano wa magari.

Ninakuhimiza kufurahia hivyo vitu vidogovidogo leo. Furahia nyumba yako, marafiki zako, watoto wako…na ndiyo, hata kwenda kazini. Kumbuka unahitaji tu kufanya uamuzi kufurahia vitu hivyo.


Sala ya Shukrani

Baba, leo ninaamua kushukuru kwa vitu hivyo vidogo na vitu vilivyopuuzwa katika maisha yangu. Nisaidie kuwa na moyo wa kutoa shukrani ambao huchagua kukuona wewe na baraka zako katika kila hali.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon