Hakikisho!

Ndiye aliye arabuni ya urithi wetu ili kuleta ukombozi wa milki yake kuwa sifa ya utukufu wake (WAEFESO 1:14)

Roho Mtakatifu ni hakikisho letu la vitu vizuri vinavyokuja. Huwa ninasema, haswa wakati ule ambao nimehisi kwamba kweli nimejazwa na Roho Mtakatifu, “Huwa vizuri sana, siwezi kufikiria jinsi utukufu wa ukamilisho mkamilifu utakavyokuwa.” Tukiwa tuna asilimia 10 (arubuni) ya kile kilicho chetu kwa sababu ya urithi wetu, hebu fikiria vile itakavyokuwa kweli kumwona Mungu uso kwa uso, kutokuwa na machozi tena, kutokuwa na majonzi, kutokuwa na mauti. Haya mawazo huniacha nikiwa nimepigwa na butwaa.

Katika Waefeso, 1:13-14, Biblia inasema kwamba, tumekwishatiwa muhuri na Roho Mtakatifu, na anatuhakikishia kwamba tutawasili salama, tukiwa tumehifadhiwa kutokana na uharibifu wote, kwenye siku ya mwisho ya ukombozi kutokana na dhambi na madhara yake yote. Hebu fikiria ajabu yake- Roho Mtakatifu ndani yetu, akituhifadhi kwa ajili ya makao yetu ya mwisho ya mapumziko, ambayo si makaburini lakini mbinguni, katika uwepo wa Mungu.

Roho Mtakatifu hutufanyia vitu vya ajabu hapa na sasa hivi. Hutuzungumzia, kutuongoza, kutusaidia, kutufundisha, kutushauri, na kutuwezesha kutimiza mipango inayosisimua ya Mungu juu ya maisha yetu, na mengine mengi. Lakini hata kama tajriba zetu naye ulimwenguni ni za ajabu, ni kionjo tu cha yale tunayoyatazamia. Tuna arubuni, lakini kuna mengine yanayokuja!

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Unaweza kuhisi salama katika kujua kwamba urithi wako huja na hakikisho.  

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon