Hakuna Asiloliweza Mungu

Hakuna Asiloliweza Mungu

Aa! Bwana Mungu, tazama, wewe umeziumba mbingu na nchi, kwa uweza wako mkuu na kwa mkono wako ulionyoshwa; hakuna neno lililo gumu usiloliweza. —YEREMIA 32:17

Katika nguvu zetu wenyewe, kuna vitu vingi ambavyo hatuwezi kutimiza. Lakini na Mungu—katika nguvu zake—vitu vyote vinawezekana. Hakuna asiloliweza Mungu wetu!

Mungu anatamani tumwamini kwa vitu vikubwa. Anataka matarajio na mipango yetu ndani yake iwe mikubwa sana hadi ituwache tumeduwaa. Tunaweza kuwa na ndoto kubwa tukiwa karibu na Mungu, kwa sababu hakuna asichoweza kufanya. Yakobo 4:2 inatuambia hatuna kwa sababu hatuombi. Tunaweza (na tunafaa) kuwa wajasiri katika kuomba kwetu.

Huenda ukafikiria, sawa, sina vipawa au talanta za kufanya mambo makubwa katika maisha yangu. Ukweli ni kwamba Mungu huwa haiti waliohitimu; huhitimisha anaowaita. Iwapo utakuwepo tu, Mungu atatumia maisha kwa njia ambazo usingedhania.

Usimwekee Mungu mipaka katika maisha yako leo. Chukua hatua ya ujasiri kwa imani na utumainie kwamba anaweza kufanya kitu kikubwa zaidi ya vile unafikiria inawezekana. Mpango wake juu ya maisha yako ni zaidi ya na juu ya vile ambavyo unaweza kuomba au hata kufikiria. Kwa hivyo sema tu kwa urahisi kwamba, “Bwana, nimefunguka kwa chochote ulicho nacho juu kwa sababu ya maisha yangu. Ninaamini kwamba utanipatia kila kitu ninachohitaji ili nitimize hiyo mipango mikubwa uliyo nayo kwa ajili yangu. Kwa jina la Yesu!”


Unapokosa kuhisi kwamba unaweza au umehitimu, mwegemee Bwana na upokee nguvu zake. Atakupa unachohitaji ili utimize zaidi ya vile ulivyodhania.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon