Kufinyangwa kwa Mfano Wake

Kufinyangwa kwa Mfano Wake

Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu. —WAFILIPI 1:6

Kulingana na Biblia, Mungu ndiye Mfinyanzi, na sisi ndio udongo (Warumi 9:20-21). Tunapokuja kwa Mungu mara ya kwanza, tunakuwa kama donge la udongo ambalo haliwezi kupindika kwa urahisi au rahisi kufanya nao kazi. Lakini Mungu hutuweka kwenye gurudumu lake la mfinyanzi na kuanza kutuunda na kututengeneza upya ili tutambue mpango mzuri alio nao juu ya maisha yetu.

Wakati mwingine huo utaratibu wa kufinyangwa hauna utulivu mara ya kwanza. Sababu inayofanya uumize ni kwa sababu lazima Mungu achambue vitu vitakavyotutenga naye katika maisha yetu. Kwa hivyo, kutokana na upendo wake kwetu, anaendelea na kuendelea kutufanyia kazi, akipuna mawazo mabaya na hiyo nia isiyo sawa, akituumba tena upya kwa uangalifu hadi polepole tubadilishwe na kufanana na Mwanawe.

Usijikatishe tamaa kwa sababu bado hujawasili. Kadri Mungu anavyofanya kazi zaidi katika maisha yako, ndivyo unavyomkaribia katika uhusiano wako naye. Furahia siku yako kila siku, hata Mungu anapoendelea kukuunda upya. Acha Mfinyanzi afanye kazi yake, na uamini kwamba ana maslahi yako mema moyoni.


Unaweza kuamini Mungu wakati wote kwamba ana maslahi yako mema moyoni, na kila afanyacho maishani mwako ni kwa faida yako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon