Kuvuta Nguvu za Mungu

Kuvuta Nguvu za Mungu

…Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. —WAEFESO 6:10

Siri muhimu katika kuwa na mafanikio katika kazi yoyote ambayo imewekwa mbele yako ni kuvuta nguvu za Mungu. Nguvu zako bila shaka zitaisha, lakini nguvu za Mungu hazitawahi kuisha.

Katika maisha yangu mara nyingi nimekuwa katika hali bila kujua nitakalofanya, lakini Mungu alikuwa akinisaidia nyakati zote na kunipitisha hadi mahali pa ushindi. Kila wakati alikutana nami na nguvu zake ambazo nilihitaji vibaya ili kuwa na mafanikio. Unaweza kumtarajia Mungu kukufanyia jambo lilohilo pia hata kama unakabiliana na changamoto gani sasa hivi. Mungu ndiye nguvu zako!

Katika Waefeso 6:10, Paulo anatuhakikishia kwamba Mungu ataachilia nguvu katika maisha yetu tunapoendelea kuishi katika uhusiano wa karibu naye. Na Nabii Isaya anasema waliojifunza siri ya kumngoja Bwana “watapaa kwa mabawa kama tai” (Isaya 40:31). Haya maandiko, na mengine kama hayo, yanatuonyesha kwamba tunatiwa nguvu tunapoenda kwa Mungu kwa ajili ya kile tunachokosa.

Mungu ameahidi kwamba hatawahi kutusahau wala kutuacha. Yuko nasi katika kila hatua ya safari yetu na hutupatia nguvu tunazohitaji kila mara tunapozihitaji.


Mungu anataka kufanya mengi zaidi ya kukupa nguvu— Anataka kuwa nguvu zako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon