Hakuna Kukosa Usalama Tena

Hakuna Kukosa Usalama Tena

Nao wakujuao jina lako wakutumaini wewe, maana wewe Bwana hukuwaacha wakutafutao. —ZABURI 9:10

Kila mmoja wetu amewahi kukosa usalama. Wakati mmoja au mwingine, sisi wote tumewahi kutaka kuchukua hatua na kufanya kitu, lakini tunapofikiria kufanya hivyo, ukosefu wa usalama unatugandisha katika jitihada zetu. Lakini huu sio mpango wa Mungu juu ya maisha yetu. Anataka tuchukue hatua kwa imani na ujasiri.

Ukosefu wa usalama hujaribu kututesa ili tuwe na tujawe na shaka na dhiki hadi tuzuiwe kufanya kile Mungu anataka tufanye na kupokea vyote ambavyo Mungu ametuwekea.

Tunaweza kuishi kwa kuwa na usalama kwa kujenga imani yetu kwa kile Mungu amesema katika Neno lake. Tunapofungua vinywa vyetu na kukiri kile Mungu anasema juu yetu na kutuhusu, Neno la Mungu litatupatia uwezo wa kushinda hofu, ukosefu wa usalama, na kukosa uhakika.

Ukijipata ukijaribu kuepuka kukabiliana na suala fulani katika maisha yako kwa sababu ya kuogopa au kukosa usalama, ninakuhimiza kuomba na kumwambia akufanyie kile alichoahidi katika Neno lake—kukutangulia na kutengeneza njia.


Mwombe Mungu amtie nguvu mtu wako wa ndani, ili nguvu na uweza wake ukujaze, na kwamba usije ukakubali kujaribiwa kuwa na woga.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon