Haujachelewa

Haujachelewa

Uwe hodari, tukajitie moyo mkuu kwa ajili ya watu wetu, na kwa ajili ya miji ya Mungu wetu; naye Bwana afanye yaliyo mema machoni pake. 1 MAMBO YA NYAKATI 19:13

Kweli unafanya unachoamini kuwa unafaa kuwa unafanya katika mahali hapa pa maisha yako, au umeruhusu hofu kukuzuia kujaribu vitu vipya—au labda viwango vya juu vya vitu vikuukuu? Iwapo hupendi jibu lako, acha nikupe habari fulani njema: haujachelewa!

Shukuru kuwa hauhitaji kuishi siku moja zaidi katika maisha ya shida ambayo yanadhibitiwa na hofu zako. Unaweza kufanya uamuzi sasa hivi kwamba utajifunza kuishi kwa ujasiri, hima, na imani. Huhitaji kuacha hofu ikutawale zaidi. Ni muhimu kukumbuka kuwa huwezi tu kukaa hapo ukingoja hofu kwenda. Kuna wakati ambapo utahisi woga huo, hata hivyo, itakubidi uchukue hatua. Ujasiri sio kutokuwepo kwa woga; ujasiri ni kuchukua hatua hata woga ukiwepo.


Sala ya Shukrani

Baba, ninashukuru kwamba sihitaji kuishi kwa hofu. Ninaomba kwamba utanijaza nguvu zako na ujasiri ili nijikaze na kushinda hofu yoyote au dukuduku ambayo huenda nikakumbana nayo leo.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon