Imani ndiyo Kiuasumu

Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi.. —2 TIMOTHEO 1:7

Iwapo unakabiliana na wasiwasi, shaka, fadhaa, au hofu katika eneo lolote la maisha yako, imani ndiyo kiuasumu.

Lifikirie hivi: Iwapo mimi ama wewe tungekunywa aina fulani ya sumu, tutahitaji kiuasumu mara moja. Jambo hilohilo ni kweli tunapokabiliana na sumu za shaka, wasiwasi, fadhaa na hofu. Lazima pawe na kiuasumu kilichopokewa—na hicho kiuasumu ni imani.

Hawa wezi wa furaha wanapokuja kubisha milangoni petu, tunaweza kujibu na imani, tukijua kwamba imani yetu ndani ya Mungu hushinda adui na itatuvuta zaidi karibu na Mungu na kuturuhusu tupumzike na kupata usalama ndani yake.

Yakobo 1:5–7 inatwambia kwamba tukijipata tukihitaji kitu, tunaweza kuomba kwa amani, na Mungu atatujibu bila kutafuta makosa. Hili ni rahisi lakini muhimu sana. Hata kama hatujakuwa watimilifu katika njia zetu, tunachoweza kufanya ni kumwomba Mungu kwa imani, na atatusaidia!


Tia imani yako ndani ya Bwana. Ana nguvu za kukukomboa na kuanzisha mwelekeo mpya katika maisha yako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon