Je, Unataka Kupona?

Je, Unataka Kupona?

Na hapa palikuwa na mtu, ambaye amekuwa hawezi muda wa miaka thelathini na minane. Yesu alipomwona huyu amelala, naye akijua ya kuwa amekuwa hali hiyo siku nyingi, alimwambia, wataka kuwa mzima? —YOHANA 5:5– 6

Si hili ni jambo la ajabu Yesu kumwuliza huyu mwanamume maskini ambaye alikuwa ameugua kwa muda mrefu wa miaka thelathini na nane: “Unataka kupona kweli?” Hilo ni swali la Bwana kwa kila mmoja wetu pia.

Unajua kuna watu ambao kwa kweli hawataki kupona? Hutaka tu kuzungumza kuhusu shida yao. Tunafaa kujiuliza iwapo tunataka kupona kweli, au kama shida yetu imekuwa kitambulisho chetu. Wakati mwingine huwa na uraibu wa kuwa na shida. Inakuwa kitambulisho chao, maisha yao. Inadhibiti kila kitu wanachofikiria, kusema na kufanya. Utu wao wote unaizunguka hiyo hiyo shida hiyo.

Iwapo una “kasoro ya ndani kabisa ya muda mrefu,” Bwana anataka ujue kwamba, si lazima iwe kitovu cha kuwepo kwako ulimwenguni. Anataka umwamini na kushirikiana naye anapokuongoza katika ushindi juu ya shida hiyo kutoka hatua moja hadi nyingine.

Hata tuwe na shida gani, Mungu ameahidi kukutana na hitaji letu na kutulipa kwa madhara tuliyopata katika siku zilizopita. Kukabili ukweli ndio ufunguo wa kufungua milango ya jela ambayo huenda imetufunga katika utumwa.


Mungu anatamani kukuona ukija kuwa vile alikupangia kuwa.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon