Jifunze Kufahamu

Naam ukiita busara, na kupaza sauti yako upate ufahamu, ukiutafuta kama fedha, na kuutafutia kama hazina iliyositirika, ndipo utakapofahamu kumcha Bwana na kupata kumjua Mungu (MITHALI 2:3-5)

Ufahamu ni kitu tunachoweza kutarajia tunapoendelea kukua na kusonga karibu na Mungu. Unatuwezesha kupenya kwenye kiini cha kitu na kuona maeneo ya ndani kabisa ya kitu hicho. Vitu haviko jinsi vinavyoonekana machoni, kwa hivyo ufahamu ni kitu cha thamani cha kuwa nacho. Tukiwa na mawazo na mioyo iliyo na ufahamu, tutajiepusha na mashaka mengi. Ninakuhimiza uombe kuwa na ufahamu kila mara.

Tukifanya uamuzi wetu kulingana na jinsi mambo yaliyvo, tunavyofikiria, au tunavyohisi, tutafanya uamuzi mwingi usiokuwa wa hekima. Kitu kinaweza kuonekana kuwa kizuri ilhali mle ndani kabisa unahisi kuwa unafaa kujihadhari na kutoendelea nacho. Iwapo ndivyo unavyohisi basi unahitaji kungoja na kuomba zaidi, ukimwuliza Mungu kukuongoza kwa Roho wake kwa kukupa ufahamu katika roho yako. Usiwahi kufanya kitu kama huna amani kukihusu au kisipotuliza roho yako.

Andiko letu la leo linatuhimiza kufahamu kumcha Mungu. Kuwa makini kutoenda kinyume na kile unahisi moyoni mwako ni wewe kufanya mazoezi ya kumcha Mungu. Ni kudhihirisha heshima kwa kile unachoamini kwamba anakuonyesha hata ingawa huenda akili zako zisikielewe kabisa. Kujifunza kuongozwa na roho ni kujifunza kuanzisha na kuheshimu vile Mungu huzungumza kila mara, ambapo ni kupitia ufahamu, kwa hivyo endelea kuomba na kufanya mazoezi katika eneo hili.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Usifanye uamuzi kulingana na maarifa ya kiakili peke yake. Fanya ukaguzi wa ndani na utazame kile ambacho ufahamu unataka kukuambia.   

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon