Jiunge na Chama

Jiunge na Chama

Moyo wa furaha huchangamsha uso; bali kwa huzuni ya moyo roho hupondeka. MITHALI 15:13

Yesu alipoalika watu kuwa wanafunzi wake na kumfuata, aliwauliza iwapo walitaka kujiunga na chama chake. Ninatambua kuwa alikuwa akiongea kuhusu kikundi chake, lakini ningependa kufikiri kwamba safari na Yesu ilikuwa ya raha na pia yenye kazi ngumu.

Mara nyingi katika injili, tunaona Yesu akialika watu kuacha maisha walioishi na kujiunga na chama chake, na bado anatoa mwaliko huo leo. Ndiyo, kuna kazi ya kufanyia ufalme wa Mungu, lakini tunashukuru kwamba tunaweza kuwa na raha huku tukiifanya.

Tunapomfuata Yesu, hatuendi katika mkutano wa heshima au matanga. Tunajiunga na chama chake ambacho kimejaa uzima, amani na furaha isiyoisha!


Sala ya Shukrani

Baba, nisaidie kuweka kando mizigo na shughuli za hii dunia na kupokea furaha yako leo. Ninakushukuru kuwa unataka nipate raha na nifurahie maisha ambayo umenipa. Kwa usaidizi wako, nitasherehekea wema wako katika maisha yangu leo na kila siku.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon