Jizoeshe Kuwa na Mtazamo Chanya

Jizoeshe Kuwa na Mtazamo Chanya

Moyo uliochangamka ni dawa nzuri; bali roho iliyopondeka huikausha mifupa. MITHALI 17:22

Ninakuhimiza kuwa mwenye shukrani na fikra chanya. Iwapo hauko hivyo, litakuwa tu jambo la kuunda desturi mpya.

Nilikuwa na fikra hasi wakati mmoja katika maisha yangu kiasi kwamba hata kama ningejaribu kufikiria fikra mbili chanya zikifuatana mfululizo, akili zangu zilionekana kukoma kufanya kazi. Lakini sasa nina fikra chanya na kwa kweli sifurahii kukaa na watu wenye fikra hasi.

Iwapo bado hujaanzisha desturi ya kuwa na fikra chanya, unaweza kuanza leo! Weka kitu cha kukukumbusha katika nyumba yako au ndani ya gari lako, ishara ndogo zinazosema, “Kuwa chanya.” Muombe Roho Mtakatifu akukumbushe ukianza kuteleza na kuingia kwenye uhasi. Waombe rafiki zako wakusaidie pia. Tenga muda mchana kuwaza kuhusu mambo mazuri ambayo Mungu amekufanyia na uwe mwenye shukrani tele kwa ajili ya vitu vingi ambavyo Mungu amekubariki navyo.

Fikra chanya zilizojaa shukrani haziji kiajali; unaweza kuchagua kujizoesha kuwa nazo. Na kumbuka, mazoezi huleta utimilifu.


Sala za Shukrani

Asante, Baba, kwa kunisaidia kuwa na fikra chanya. Nina furaha kwamba mimi si mfungwa wa mawazo hasi na kwamba ninaweza kuchagua kufurahi na kujawa na furaha.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon