Kama ulivyoamini

Kama ulivyoamini

Naye Yesu akamwambia yule akida, Nenda zako; na iwe kwako kama ulivyoamini. Mtumishi wake akapona saa ile ile. Mathayo 8:13

Miaka mingi iliyopita nilikuwa mbaya sana kwa sababu ya unyanyasaji mkubwa uliofanyika katika siku zangu zilizopita. Matokeo yake ni kwamba nilitarajia watu kunidhuru, na walifanya hivyo. Nilitarajia watu kutowa waaminifu, nao walikuwa hivyo. Niliogopa kuamini kwamba chochote kizuri kinaweza kutokea.

Nilidhani nilikuwa najilinda kutokana na kuumizwa kwa kutotarajia kitu chochote kizuri kutokea. Lakini wakati nilipoanza kujifunza Neno na kumtegemea Mungu kurejesha maisha yangu, nilianza kutambua kwamba kutojipenda kwote kulipaswa kwenda.

Katika Mathayo 8:13, Yesu anasema kwamba itafanyika kwetu kama tulivyoamini. Niliamini kila kitu kilikuwa kibaya, kwa hivyo mambo mengi mabaya yaliyotokea kwangu. Niliamua nilitaka mambo mazuri yatendeke kwangu, kwa hiyo nikaanza kuweka imani yangu kwa Mungu, nikiamini kuwa atafanya mambo mazuri katika maisha yangu, na baada ya muda, nilipokea matokeo mazuri!

Je, unakabiliwa na mambo mabaya na unashangaa kwa nini? Labda unahitaji kuanza kuamini mambo tofauti. Anza kumtegemea Mungu na kuamini kwa mambo bora. Kisha angalia huku akikufanyia mambo kulingana na imani yako.

OMBI LA KUANZA SIKU

Roho Mtakatifu, nataka kuondokana na upotevu wote na kuanza kuamini kwa mambo mazuri. Nisaidie nisisitize imani yangu, naamini kwamba Unaweza kufanya mambo makuu katika maisha yangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon