
Naye Bwana, yeye ndiye atakayetangulia, atakuwa pamoja nawe, hatakupungukia wala kukuacha; usiogope wala usifadhaike. KUMBUKUMBU LA TORATI 31:8 BIBLIA
Hofu ni roho inayozalisha hisia. Mungu alipomwambia Yoshua kutoogopa, hakuwa akimwamrisha “kutohisi” hofu; alikuwa akimwamrisha kutokubali hofu iliyokuwa imemkabili.
Mara nyingi huwa ninawahimiza watu “fanya ukiwa na hofu.” Kimsingi hiyo inamaanisha hofu inapokushambulia, unahitaji tu kuendelea kufanya kile Mungu anakuambia ufanye. Huenda ukakifanya huku magoti yako yakitetemeka au viganja vyako vikitoka jasho, lakini hata hivyo fanya tu. Hiyo ndiyo maana ya “usiogope.”
Tunaweza kushukuru kuwa tuna Andiko ili kutafakari tunapohisi woga. Ahadi za Mungu hututia nguvu ili tuendelee kukaza mwendo, bila kujali tunavyohisi. Neno la Mungu litakupa imani unayohitaji ili kushinda hisia yoyote ya woga.
Sala ya Shukrani
Asante, Baba, kwamba si lazima nishindwe na hisia ya woga. Kwa usaidizi wako, ninaweza kukaza mwendo na kufanya kile umeniita kufanya bila kujali hisia zangu. Asante Baba kuwa ninaweza kukifanya nikiwa mwoga.