Kiwango Kipya cha Uwajibikaji

Kiwango Kipya cha Uwajibikaji

Umkabidhi Bwana njia yako, pia umtumaini, naye atafanya. ZABURI 37:5

Mungu anataka kutupeleka kwa kiwango kipya cha uwajibikaji. Hili ni jambo la kusisimua na kushukuru kwa sababu uwajibikaji huja na baraka. Si rahisi wakati wote, lakini ina faida zake. Sisi wote hupigana vita na kukabiliwa na majaribu ya kuacha kupigana na kukata tamaa tu, lakini uwajibikaji ndicho kitu kinachotuwezesha kupinga majaribu hayo.

Ukiwajibikia kwa bidii kusudi la Mungu juu ya maisha yako, utaanza kupata vyote alivyo navyo kwa ajili yako. Mungu anakupenda na anataka uwe na uhusiano wa dhati naye—kwa maisha. Sidhani kuna kitu chochote kinachoridhisha zaidi, kinacholipa zaidi au kusisimua zaidi. Amekuwekea vitu vingi kuliko vile ambavyo umewahi kuomba au kuwaza, lakini ili uone mipango yake ikifanyika katika maisha yako, utahitaji kuwajibika kwa ajili yake na hiari yake.


Sala ya Shukrani

Baba, ninachagua kukuwajibikia kikamilifu. Ninakushukuru kwamba unaniongoza katika hatma uliyoniwekea. Kwa usaidizi wako, nitakutazama wewe, na kuweka kila sehemu ya maisha yangu katika kila mpango na kusudi lako juu ya maisha yangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon