Kuangusha Ngome

Maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome. —2 Wakorintho 10:4

Kupitia kwa mikakati makini na ujanja wa udanganyifu, shetani hujaribu kujenga “ngome” katika fikra zetu. Ngome ni eneo ambapo tunatekwa nyara katika utumwa (katika jela) kwa sababu ya njia fulani ya kufikiri. Ngome ni uongo unaoaminika.

Mtume Paulo anatuambia kuwa tuna silaha za kiroho tunazohitaji ili kushinda ngome za shetani. Kwa kutumia silaha zetu, tunapinga uongo wa mwovu, ushindani, nadharia, urazini na kila kitu kinginecho ambacho hujaribu kujiinua juu ya ukweli wa Neno la Mungu. Lazima tuziteke fikra zetu nyara na kukataa kujihusisha katika tamaa za mwili za kupokea na kutafakari kila wazo linaloanguka vichwani mwetu (2 Wakorintho 10:5).

Silaha kuu ambayo huwa tunatumia kwa vita ni Neno la Mungu linalotumiwa kwa njia tofauti katika—kuhubiri, kufundisha, kuimba, kukiri, kutafakari, kuandika na kusoma.

Maarifa ya Neno la Mungu yatatusaidia kugeuza nia zetu na kutufundisha kufikiri kwa njia mpya kabisa. Litaangusha ngome ambazo zimekuwa zikituweka katika utumwa!


Kwa kweli hakuna atakayewahi kuishi maisha ya ushindi bila kuwa mwanafunzi mwaminifu wa Neno la Mungu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon