Kubarikiwa kuwa Baraka

Kubarikiwa kuwa Baraka

Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine. WAFILIPI 2:4

Kila mtu anahitaji baraka. Sisi wote tunahitaji kutiwa moyo, kuinuliwa, kusifiwa na kufurahiwa. Na una uwezo wa kubariki watu wengine. Shukuru kuwa Mungu hakubariki tu wewe lakini kuwa amekufanya baraka. Sisi wote huchoka wakati mwingine na kuhitaji watu wengine kutujulisha kuwa sisi ni wa maana na tunahitajika.

Ninaamini Mungu hutubariki ili tuweze kuwa baraka—sio tu mahali pachache lakini kila mahali tunapoenda. Tafuta watu walio na mahitaji na uwabariki. Wape ulicho nacho wale waliopungukiwa kuliko wewe. Na ukumbuke, kila mmoja anahitaji baraka—hata watu waliofanikiwa ambao huonekana kuwa na kila kitu.

Ukiishi kwa kutimiza mahitaji ya watu na kuhimiza walio karibu nawe, utapata “furaha isiyosemezeka” katika utaratibu huo (tazama 1 Petro 1:8 Biblia)


Sala ya Shukrani

Baba, ninashukuru kwa baraka zako katika maisha yangu, na ninashukuru pia kwamba umeniwezesha kuwa baraka. Nisaidie kuwafikia wengine kila siku na kuwahimiza zaidi.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon