Kuchochewa Kuchukua Hatua

Basi Musa akawaita Bezaleli na Oholiabu, na kila mtu aliyekuwa na moyo wa akili, ambaye Bwana alimtia moyoni mwake hekima, kila mtu ambaye moyo wake ulimhimiza ili aende kufanya kazi hiyo. —KUTOKA 36:2

Kitu cha nguvu hufanyika katika maisha yako moyo wako unapochochewa kuchukua hatua. Haitusadii kusema, “Oh, ninatamani ningehisi hivyo.” Tunaweza kuamua kufanya kitu kuhusu vile tunavyohisi kwa kuchochea mioyo yetu wenyewe kuchukua hatua na kufanya kile Mungu ametuita kufanya.

Tunachochea vipi imani? Nimegundua kwamba Neno la Mungu kutoka katika kinywa changu kwa njia ya maombi, sifa, kuhubiri, au kukiri Neno la Mungu ndizo njia nzuri kabisa nilizopata za kuchochea moto. Huchochea kipawa kilicho ndani, kuamsha imani na tumaini langu na kuzuia roho yangu kutokana na kuzama ndani yangu.

Ukimya, kuahirisha, na uvivu ni vifaa ambayo adui hutumia kinyume na watu wa Mungu. Mtu mtulivu hungoja kusongezwa na nguvu za kutoka nje kabla ya kuchukua hatua. Lakini tunaweza kuchochewa na kuongozwa na Roho Mtakatifu aliye ndani yetu, sio na nguvu za nje. Njia nzuri ya kujilinda kutokana na ukimya ni kufanya chochote kilicho mbele yako kwa nguvu zako zote.


Endelea kuchochea kipawa ulichopewa na Mungu, huo moto ulio ndani yako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon