Kufanya Ungamo la Imani

Kufanya Ungamo la Imani

Bwana ni mwema, ni ngome siku ya taabu; naye huwajua hao wamkimbiliao. NAHUMU 1:7

Ukichagua kuungama na kutafakari juu ya wazo, ninamwamini Mungu kabisa; hakuna haja ya kuwa na wasiwasi, utaunda fikra mpya ambazo zitakuwezesha kumwamini Mungu kwa utulivu. Utafanya desturi kutafuta yaliyo mema na kuyatukuza, huku ukishukuru Mungu kwa kila ushindi katika maisha yako. Maisha hufurahisha sana tukiamua kuomba kwa ajili ya kila kitu na kuacha wasiwasi.

Usikate tamaa iwapo kuunda fikra mpya litakuwa jambo gumu mwanzoni. Huenda utalazimika kusema mara 1000 kuwa utamwamini Mungu na hutafadhaika kabla hujaanza kuhisi athari za kufanya hivyo. Kumbuka tu kwamba kila wakati ukifikiri na kusema kitu kinachokubaliana na Mungu, unapiga hatua. Shetani atajaribu bila kuchoka kukufanya ukate tamaa, lakini kama utaamua kumwamini Mungu bila kuchoka, ninakuhakikishia kuwa utaona matokeo hivi karibuni.


Sala za Shukrani

Ninakushukuru, Baba, kwamba wewe ni mwaminifu na ninaweza kukutegemea katika kila eneo la maisha yangu. Ninaamini kwamba unaweza kushughulikia kila shida na shida zote zinazonikabili. Sitafadhaika; Nitakuamini.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon