Kufurahia Mahusiano yenye Amani na Upatanifu

Kufurahia Mahusiano yenye Amani na Upatanifu

. . . Nanyi mtanyamaza kimya … KUTOKA 14:14

Tuliumbwa kuishi katika upendo na kufurahia mahusiano yenye upatanifu, yaliyo huru kutokana na ugomvi, kuchanganyikiwa, na kiwewe cha kihisia. Mungu anataka maisha yetu kuwa huru kutokana na migawanyiko; anataka tuishi kwa amani na kila mmoja; ilhali maisha kama hayo huwakwepa watu wengi. Badala yake, ugomvi huvuruga maisha yao, na kuwaacha wakiteseka na kutengana na wengine.

Lakini tunaweza kushukuru kuwa Yesu anatupatia amani yake. Hatuhitaji kuishi na mahusiano yaliyovunjika na kujaa ugomvi. Tunaweza “kuwa na amani” katika kila hali. Zaburi 34:14 inasema tunaweza “kutafuta amani na kuifuatia” Mathayo 5:9 inasema, tunaweza kuwa “wapatanishi na wadumishaji wa amani.” Tunapokuwa na amani, Mungu hutenda kazi kwa niaba yetu.

Usiache matatizo ya mahusiano yasumbue maisha yako tena. Dhamiria kukomesha ugomvi na ufanye kila uwezalo kuifuatia amani. Ukiamua kuwa mpatanishi, utashangaa mabadiliko yatakayotokea.


Sala ya Shukrani

Baba, nisaidie kuwa mpatanishi katika mahusiano yangu. Ninakushukuru kuwa siharibu tena wakati wangu katika ugomvi juu ya mambo madogomadogo na mabishano ya kijinga. Kutegemea mimi na kwa usaidizi wako, nitakuwa na mahusiano ya amani na ulinganifu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon