Weka Lengo ili Kufurahia Kila Sehemu ya Siku Yako

Weka Lengo ili Kufurahia Kila Sehemu ya Siku Yako

Kwa hiyo moyo wangu unafurahi, nao utukufu wangu unashangilia, naam, mwili wangu nao utakaa kwa kutumaini. ZABURI 16:9

Kuna idadi kubwa ya vitu ambavyo hufanyika wakati wa maisha ya kawaida ya kila siku, na tunaweza kuvifurahia vyote iwapo tutafanya uamuzi kufanya hivyo.

Vitu kama kuvaa, kuendesha gari hadi kazini, kwenda sokoni, kujitumatuma, kupanga mambo, kutuma barua pepe, kupeleka watoto mazoezi, na mamia ya vitu vingine. Hata hivyo maisha yamejengeka kwa vitu hivyo. Anza kuvifanya kwa moyo wenye shukrani na utambue kuwa, kupitia kwa Roho Mtakatifu, unaweza kufurahia kila kitu unachofanya kila siku ya maisha yako.

Furaha haiji tu kwa kutumbuizwa, lakini kutoka kwa uamuzi wa kufurahia kila wakati ambao umepewa kama kipaji adimu na cha thamani kutoka kwa Mungu.


Sala ya Shukrani

Baba, asante kwa kipaji cha maisha, na asante kwa kila shughuli inayokuja na kipaji hicho. Ninaomba kwamba utanisaidia kupata furaha katika kila sehemu ya siku yangu ninapoishi kwa ajili yako. Ninakushukuru kwamba ninaweza kuchagua kufurahia hata shughuli za sehemu ya kawaida ya siku yangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon