Kuishi katika Neema ya Mungu

Kuishi katika Neema ya Mungu

“Naye akaniambia, neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu.” 2 WAKORINTHO 12:9 BIBLIA

Ukweli kwamba Mungu anataka ufurahie maisha yako ni baraka ambayo kila mwaminiye anaweza kushukuru kwayo. Lakini kitu kimoja kikubwa ambacho kitakuzuia kufurahia maisha yako ni kazi ya mwili. Kazi ya mwili wetu ni nguvu zetu, bidii zetu katika kujaribu kufanya tu kile ambacho Mungu peke yake anaweza kufanya.
Kujaribu kufanya kazi ya Mungu kila mara husababisha kukata tamaa. Kumwamini Mungu kufanya tu kile ambacho Yeye peke yake anaweza kufanya husababisha furaha kwa sababu “”Yasiyowezekana kwa wanadamu, yawezekana kwa Mungu” (Luka 18:27).

Biblia inasema kwamba neema ya Mungu imetutosha. Neema ni kibali cha Mungu tusichostahili na nguvu za Mungu za kutimiza mahitaji yetu na kusuluhisha matatizo yetu. Huwa tunakata tamaa tunapojaribu kufanikiwa kwa matendo, maisha ambayo Mungu alipanga tupokee kwa neema. Kwa hivyo pumzika katika neema yake leo na ushukuru kwa furaha ambayo neema inaahidi kuleta.


Sala ya Shukrani

Ninashukuru, Baba, kwa neema yako katika maisha yangu. Nisaidie kupokea neema kupitia kwa imani ndani yako kila wakati na kukuamini kufanya kile wewe peke yako unaweza kufanya.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon