Kukaa na Amani

Kukaa na Amani

Tubuni basi, mrejee ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana. MATENDO YA MITUME 3:19

Amani na Mungu hudumishwa kwa kutojaribu kuficha dhambi. Kwa sababu kuficha dhambi husababisha tu hukumu na hatia, na hakuna inayofaidisha kwa njia yoyote. Mungu anajua kila kitu hata hivyo, kwa hivyo haileti maana kufikiri tunaweza kuficha kitu chochote kutoka kwake. Tunapofanya makosa, hatufai kuondoka kwa Mungu, lakini tunafaa kuja karibu naye, tukiwa na shukrani kwamba atatuhuisha.

Kutubu inamaanisha kugeuka kutoka kwa dhambi na kurudi mahali pa juu zaidi. Mungu hashangazwi na udhaifu na kushindwa kwetu. Kweli, alijua kuhusu makosa tutakayofanya kabla tuyafanye. Kile tunachohitaji kufanya ni kuyakubali kwa sababu ni mwaminifu atatusamehe dhambi zote kila mara (tazama 1 Yohana 1:9). Mungu anakungoja kwa mikono wazi iliyonyoka—mkimibilie kila wakati!


Sala ya Shukran

Ninashukuru, Baba, kwamba unasamehe dhambi zangu na unaleta uponyaji na uhuisho katika maisha yangu. Ninachagua kukataa hukumu ya adui na kuja kwako ninapotenda dhambi na kupungukiwa. Asante kwa kuwa huwa unanisamehe na kunipenda wakati wote.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon