Kununuliwa Kwa Damu Ya Yesu

Kununuliwa kwa Damu ya Yesu

Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, msamaha wa dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake. —WAEFESO 1:7

Jisemee kwa sauti, “Nilinunuliwa na kusafishwa kutokana na dhambi kwa gharama; kununuliwa kwa thamani; kulipiwa na kumilikiwa na Mungu.” Umeokolewa kutokana na dhambi pamoja na “mauti” yote inayoleta.

Wasiwasi, fadhaa, na hofu ni aina za mauti. Ugomvi, uchungu, hasira, na kutosamehe ni aina za mauti. Damu ya Yesu ndiyo dawa pekee ya mauti.

Damu ya Yesu ni ya thamani mbele za Baba na inafaa kuwa yenye thamani kwetu. Kitu chenye thamani ni kitu tunachokinga, kitu tunachotunza sana na kitu ambacho hatutaki kukiacha.

Damu ya Yesu ni yenye thamani na huturuhusu kuwa karibu na Baba yetu wa mbinguni. Dhabihu yake iliondoa veli iliyokuwepo baina ya Mungu na mwanadamu, na sasa tuna uhuru wa kumfikia, na tuna nafasi ya ukaribu na undani na Mungu (Waebrania 10:18-22).

Damu ya Yesu hutusafisha kutokana na dhambi na itaendelea kutusafisha (1 Yohana 1:9). Damu yake ni kama dawa kali ya kusafishia. Vile tu damu yetu inavyofanya kazi kusafisha miili yetu kutokana na sumu yote, kila wakati, damu ya Yesu hutusafisha kutokana na dhambi za aina zote pamoja na dalili zake.


Kuwa na imani katika nguvu za damu ya Yesu kukusafisha kila mara kutokana na dhambi katika aina zake zote pamoja na dalili zake.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon