…na mwingine kupambanua roho… (WAKORINTHO 12:10)
Ninaamini kupambanua roho ni karama ya thamani sana, na ninakuhimiza kuitamani na kuikuza. Watu wengine husema kwamba kupambanua roho huwapa watu utambuzi wa kiungu wa ulimwengu wa kiroho Mungu anaporuhusu. Wengi pia wanaamini kwamba kupambanua kwa roho ni karama iliyotolewa ili tujue asili ya ukweli ya mtu au hali. Ulimwengu wetu umejaa udanganyifu na watu wengi hawako vile wanavyoonekana kuwa. Karama ya kupambanua roho hutusaidia kuona mambo ambayo watu huficha ili tujue kinachoendelea haswa. Hiyo karama hutusaidia pia kuhisi wakati ambapo kitu ni kizuri au mtu ana roho nzuri.
Dave na mimi tumeona karama hii ikifanya kazi mara nyingi tunapoajiri watu wa kufanya kazi katika huduma yetu. Mara nyingi watu wameonekana kuwa wenye wamehitimu, wanaoweza, waliojitolea, na “watimilifu” kwa kazi ambazo waliomba nafasi ya kuzifanya. Ninakumbuka wakati mmoja tulipokutana na mtu fulani na kila mtu aliyehusika akafikiri tumwajiri, lakini nilikuwa na hisia iliyonisumbua moyoni mwangu kwamba tusifanye hivyo. Tulimwajiri hata hivyo na hakufanya lolote isipokuwa kuzua mashaka. Niliruhusu fikra zangu kwenda kinyume na upambanuaji wangu wa roho na ninajuta kwamba tusingemwajiri– nikifikiri atafanya kazi kwa sababu wasifu kazi yake ndiyo tulitaka haswa.
Roho wa Mungu huishi katika mioyo yetu na kuzungumza na mioyo yetu, sio vichwa vyetu. Karama zake si za kiakili au hazitumikishwi katika nia zetu; ni za kiroho na hutumikishwa katika roho zetu. Lazima tufuate tunachohisi katika roho zetu, sio kile tunachofikiri katika mawazo yetu kwamba ndicho sawa. Ndiyo kwa sababu Mungu hutupa upambanuaji.
NENO LA MUNGU KWAKO LEO:
Jifunze kupambanua na usifanye uamuzi unaotegemea unachoona na kufikiria.