Kupata Hekima katika Kiasi

Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa. —YAKOBO 1:5

Magurudumu ya gari lako yakikosa kiasi, utakuwa na mwendo wa kudundadunda. Ninafikiri kitu hichohicho kinaweza kufanyika maishani mwetu. Tukiondoka katika kiasi kwenye eneo moja au zaidi, safari ambayo ingekuwa nyororo inakuwa na kudundadunda na isiyotuliza.

Inawezekana kupita mipaka na kutoka kwenye kiasi katika eneo lolote la maisha—hata maeneo mazuri kabisa. Mwanamke anaweza kuharibu ndoa yake kwa kuzingatia watoto. Akitumia kila muda na nguvu zake zote kwa kushughulikia watoto lakini akose kutambua mahitaji ya mume wake, ndoa yake itatatizika.

Wanaume (na wanawake wengi pia) huzama katika kazi zao. Iwapo mwanamume atatumia wakati wake wote kazini, na kumtelekeza mkewe na watoto, huenda akawa mpaji mzuri, lakini ana upungufu kama mume na baba. Kiasi ni muhimu.

Huu ni ukweli hata katika maeneo madogo. Watu wengine huzungumza kwa nadra, na wengine huzungumza sana. Watu wengine hufanya mipango mingi kupita kiasi, na wengine hawafanyi mipango yoyote. Wakati mwingine tunakuwa na mawazo ya juu kujihusu, na wakati mwingine tunakuwa na mawazo duni sana kujihusu. Hata vitu hivyo vidogo vinaweza kutoka kwenye kiasi.

Chunguza maisha yako kwa uaminifu na uone iwapo kuna eneo ambalo uko nje ya kiasi. Mwombe Mungu hekima ya kufanya marekebisho yanayohitajika ili uishi maisha ya kiasi yenye afya, na yaliyojaa furaha.


Ukimwomba Mungu hekima, anakupatia.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon