Kupata Ujasiri wa Kuwa wa Kipekee

Kupata Ujasiri wa Kuwa wa Kipekee

Wala si kwa utumwa wa macho tu wajipendekezao kwa wanadamu bali kama watumwa wa Kristo, mkitenda yapendezayo Mungu kwa moyo. —WAEFESO 6:6

Ili kuwa mtu uliyeitwa kuwa ndani ya Yesu, kuchagua kuishi kwa ujasiri kwa uhusiano wa karibu na Mungu, ni muhimu uwe na ujasiri wa kuwa wa pekee. Hiyo ina maana ya kuridhika na vile Mungu alikuumba, kuchagua kutokuwa kama kila mtu.

Mojawapo ya mitego rahisi ambayo tunaweza kuingia ni mtego wa kuwa “mpendeza binadamu.” Lakini kujaribu kupendeza wengine hatimaye husababisha masikitiko. Mara ya kwanza tunapoanza kubadilisha nafsi zetu ili kupendeza watu wengine, huwa tunasikia maoni yanayotufanya tuhisi vizuri. Lakini hili halitadumu. Maoni ya watu ni bandia na hubadilikabadilika kila mara. Ni maoni ya Mungu tu yaliyo muhimu.

Wewe unastahili kwa sababu Mungu alimtuma Mwanawe wa pekee kufa kwa ajili yako. Unafaa kwa sababu Mungu anakupenda, sio kwa sababu ya vile mtu mwingine anafikiria kukuhusu au anasema kukuhusu.

Ninakuhimiza kukumbatia vitu ambavyo vinakufanya uwe wa pekee. Iwapo nywele zako ni tofauti kidogo, iwapo roho yako ni ya kipekee, iwapo talanta yako ni ya kipekee—chochote kile, shukuru Mungu kwamba alikuumba kwa njia spesheli na uchague kutumia vipawa na talanta zako na nafsi yako kwa utukufu wa Mungu.


Ni wakati ule tu ambao unakumbatia mtu ambaye Mungu alikuumba kuwa ndio unafurahia maisha ambayo Yesu alikufa kukupa.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon