Kupatana na Watu Wasumbufu

Kupatana na Watu Wasumbufu

Kama yamkini, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote. WARUMI 12:18

Unakabiliana vipi na watu wajeuri? Je, unawajibu kwa upendo vile Neno linavyosema kuwa tunafaa, au unaungana nao katika tabia zisizo za kiungu? Ninafikiri kuna watu wengi wajeuri na wasiofurahisha ulimwenguni leo hususan kwa sababu ya maisha ya mfadhaiko ambayo watu wengi huishi.

Tunaweza kushukuru sana kwamba tunajua Neno la Mungu na tunaye katika maisha yetu kutusaidia na kutufariji—kutuzuia kuingia katika majaribu ambayo mfadhaiko unaweza kusababisha. Lakini lazima tukumbuke kuwa watu wengi ulimwenguni ambao ni wagumu kupatana nao hawana subira. Yesu alisema hatutakuwa tumefanya chochote maalum iwapo tutawatendea wema wanaotutendea mema lakini tukiwapenda adui zetu basi tumetenda wema (tazama Luka 6:32–35).

Watu wako kila mahali, na sio wote wanafurahisha. Je, utalitenda Neno la Mungu kwa kuwapenda kwa ajili yake?


Sala ya Shukrani

Baba, nikiwa katika hali ambayo inanihitaji kukabiliana na mtu mgumu wa kupatana naye, niache niwaombee badla ya kuwakasirikia. Asante kwa kunipa neema ya kuwa mkarimu kwa kila mtu—bila kujali wanavyonitendea.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon