Kupenda Watu, Kuamini Mungu

Kupenda Watu, Kuamini Mungu

Lakini Yesu hakujiaminisha kwao; kwa kuwa yeye aliwajua wote; na kwa sababu hakuwa na haja ya mtu kushuhudia habari za mwanadamu; kwa maana yeye mwenyewe alijua yaliyomo ndani ya mwanadamu. YOHANA 2:24–25

Yesu aliwapenda watu—tunaona hilo katika utangamano wake na watu, haswa wanafunzi wake. Alikuwa na ushirika mkuu nao—alisafiri nao, akala nao, na kufundisha nao—lakini hakujiaminisha kabisa kwao. Kwa sababu alijua yaliyomo ndani ya mwanadamu.

Hiyo haina maana kwamba hakuwaamini kamwe; ina maana kuwa hakujifungua na kujipeana kwao vile alivyomwamini Mungu na kujifungua kwa Baba yake wa mbinguni. Hakuwatarajia kuwa watimilifu kwake na kutomsikitisha.

Tunaweza kushukuru kwa mfano wa Yesu kwa sababu anatuonyesha vile tunafaa kuishi. Tunafaa kupenda watu, na tunaweza kuwaamini, lakini tusiwaamini kama vile tunavyomwamini Mungu. Yeye huwa mwaminifu kila wakati, na huwa na maslahi yako mema moyoni mwake.


Sala ya Shukrani

Baba, asante kwa mfano wa Yesu. Ninapenda na kuwaamini watu walio karibu nami maishani, lakini tegemeo na tumaini langu la mwisho liko ndani yako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon