Kupumzika Ndani ya Bwana

Kupumzika Ndani ya Bwana

Akasema, uso wangu utakwenda pamoja nawe, nami nitakupa raha. KUTOKA 33:14

Tunaweza kuwa wenye shukrani kwamba si lazima tuwe na wasiwasi kuhusu vitu, kufikiria au kubeba mizigo mizito katika maisha yetu. Kwa kweli ni jambo la kuburudisha sana—na kitu cha kushukuru kwacho—kutambua kwamba sihitaji kuwa na majibu yote kwa shida zangu. Tunahitaji kutulia na kusema, “Sijui jibu la huu mtanziko, na sitakuwa na wasiwasi kuhusu lolote kwa sababu Mungu anatawala na ninamwamini. Nitatulia ndani yake!”

Tunapolemewa na mizigo ya maisha—kung’ang’ana, kufanya kazi, na kufadhaika—tunahitaji likizo ya kiakili na kihisia. Akili zetu zinahitaji kupumzika kutoka kwa kuwa na mfadhaiko. Wasiwasi haina utulivu kabisa. Kwa kweli huiba utulivu na faida za utulivu kutoka kwetu. Kwa hivyo wakati ujao ukihisi umebeba mzigo mzito katika moyo wako au ujipate una wasiwasi na mfadhaiko, kumbuka, unaweza kuweka tumaini lako ndani ya Mungu na kufurahia utulivu wake.


Sala ya Shukrani

Baba, ninashukuru kwamba unanipa utulivu. Asante kwa kuwa sihitaji kuwa na majibu yote kila wakati—ninaweza kukuamini na niishi maisha ya amani, ridhaa na utulivu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon