Zaidi ya Kusamehewa Nusu…Kusamehewa Kikamilifu

Zaidi ya Kusamehewa Nusu…Kusamehewa Kikamilifu

Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli. YOHANA 8:36 BIBLIA

Shetani hukumbuka kila kitu kidogo ambacho tumewahi kukosea na atafanya awezalo kutukumbusha vitu hivyo kila anapopata nafasi. Ana bidii katika juhudi zake za kutufanya tuiname chini ya uzito wa aibu zetu wenyewe. Sisi wote hutenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu. Hakuna mtu asiye na dhambi, na sisi wote huhisi kuhukumika wakati mwingine, lakini tukiweka hiyo hukumu muda mrefu baada ya kusamehewa, inabadilika na kuwa aibu.

Hukumu na aibu hutufanya tuhisi kwamba Mungu ana hasira, na kwa hivyo tunaondoka katika uwepo wake na kutoishi maisha ambayo alikusudia tuishi. Tunahitaji kuelewa na kushukuru kuwa Mungu hutusamehe kikamilifu—sio nusu, au karibu, lakini kikamilifu! Wema wa Mungu ni mkuu kuliko kitu chochote kibaya ambacho tumewahi au tutawahi kufanya. Hilo linafaa kuleta hisia ya shukrani au hisia za furaha zikibubujika katika mioyo yetu!


Sala ya Shukrani

Baba, ninashukuru kwamba unanisamehe dhambi zangu kikamilifu ninapoomba msamaha. Bila kujali nililofanya, msamaha umefanikishwa kupitia kwa dhabihu ya Yesu. Asante kwa kuwa mimi ni mwenye haki machoni mwako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon