Kutayarishwa kwa Furaha

Kutayarishwa kwa Furaha

Matumaini yao wenye haki yatakuwa furaha; bali kutaraji kwao wasio haki kutapotea. MITHALI 10:28

Tunaweza kushukuru kwamba ni mapenzi ya Mungu kwetu kufurahia maisha aliyotoa. Furaha ya Mungu ni nguvu zetu. Tukiwa na ufahamu huo, tunaweza kufanya uamuzi wa kufurahia maisha kila siku.

Kufurahia maisha haina maana kuwa tuna kitu kinachosisimua ambacho kinaendelea kila wakati; inamaanisha kufurahia tu vitu rahisi vya kila siku. Aghalabu maisha huwa ni ya kawaida, lakini tumetayarishwa kwa njia isiyo ya kawaida kwa nguvu za Mungu kuishi maisha ya kawaida ya kila siku kwa njia isiyo ya kawaida.

Ndiyo, inachukua nguvu za Mungu kufurahia maisha kwa sababu maisha yote si rahisi. Vitu vingi ambavyo hatujapanga hufanyika, na vingine ni vigumu. Lakini Yesu alisema, “Changamka, nimeushinda ulimwengu, na kuchukua nguvu zake za kukudhuru” (tazama Yohana 16:33).


Sala ya Shukuru

Baba, nikikabiliwa na hali ngumu, nisaidie kuchagua furaha bila kujali hali yangu. Ninakushukuru kwamba furaha yako ni nguvu yangu kila siku.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon