Kutoka Shimoni hadi Kwenye Kasri

Kutoka Shimoni hadi Kwenye Kasri

Farao akamwambia Yusufu, kwa kuwa amekufahamisha hayo yote, hapana mwenye akili na hekima kama wewe. Basi wewe utakuwa juu ya nyumba, na kwa neno lako watu wangu watataliwa. Katika kiti cha enzi tu nitakuwa mkuu kuliko wewe. —MWANZO 41:39–40

Shimo ni mtaro, mtego au kitanzi. Linarejelea uharibifu. Mara nyingi shetani hutaka kutuleta shimoni.

Yusufu aliuzwa utamwani na ndugu zake. Kwa kweli walimtupa shimoni na kukusudia kumwacha mle kufa, lakini Mungu alikuwa na mipango mingine. Yusufu akaishia kuuzwa utumwani Misri, ambako alitupwa jela kwa kukataa kulegeza maadili yake. Ilhali kila Yusufu alikoenda, Mungu alimpa kibali. Mwisho wa yote, Yusufu alipandishwa cheo hadi kwenye kasri, kama mdogo wa Farao.

Yusufu alitoka vipi katika shimo hadi kwenye kasri? Ninaamini ni kwa kubaki na fikra nzuri, kukataa kuwa na uchungu, na kuchagua kumtumainia Mungu kwa ujasiri. Hata ingawa alionekana kushindwa wakati mwingi, alikataa kukata tamaa ya kumwamini Mungu.

Yusufu alikuwa na fikra nzuri. Alijua kwamba Mungu alikuwa katika usukani hata kama hali ya maisha yake ilionekana kuyumbayumba bila kudhibitika. Hilo pia ni kweli kuhusu maisha yako. Iwapo utakuwa na fikra nzuri, ukijua kwamba Mungu yuko usukani, anaweza kukutoa shimoni na kukupeleka kwenye kasri katika njia ambazo hujawahi kufikiria.

Haijalishi ulikoanzia, unaweza kuwa mwisho mkuu!

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon