Unaweza Kuwa Karibu na Mungu Kadri Unavyotaka

Unaweza Kuwa Karibu na Mungu Kadri Unavyotaka

Mungu amesema, “Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa.” WAEBRANIA 13:5 BIBLIA

Kujenga urafiki wako na Mungu ni sawa na kujenga urafiki wako na mtu hapa duniani. Ukweli ni kwamba unaweza kumkaribia Mungu kadri unavyotaka; yote yategemea wakati ambao unahiari kuwekeza katika uhusiano huo. Ninakuhimiza kumjua kwa kutenga muda wa kuomba na kusoma Neno na kwa kumhusisha katika vitu vyote unavyofanya.

Urafiki wako na Mungu utakuwa wa ndani sana na kukua unapotembea naye na kuona uaminifu wake. Anzisha desturi ya mazungumzo rahisi ya upendo kila mara na Mungu. Yuko na wewe kila wakati na yuko tayari kukusikiza kila wakati. Ni rafiki ambaye hatakuacha wala kukupungukia. Ambaye ni mwaminifu, mwenye kutegemewa, mwenye upendo, na msamehevu. Huyo ni rafiki tunayeweza kushukuru kwa ajili yake!


Sala ya Shukrani

Baba, ninakushukuru kwamba uhusiano wangu na wewe unajengeka na kuimarika kila siku. Asante kwa kuwa wewe ni wa kutegemea na hutanisikitisha.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon