Kuwa Mwenye Bidii katika Maombi

Ijapokuwa naliwaombea (ZABURI 109:4)

Maombi yanaweza kuwa mafupi na bado yawe na athari, lakini hilo halimaanishi kuwa misimu mirefu ya kuzungumza na kusikiliza Mungu si muhimu na yenye thamani. Bila shaka ni muhimu. Kwa kweli, kando na maombi ya kila siku, ninapendekeza kutenga siku nzima au hata siku kadhaa mtawalia nyakati chache kwa mwaka zitengwe tu kwa lengo la kumtafuta Mungu katika maombi na kusoma Neno lake. Nyakati za kufunga zinaweza pia kuwa za manufaa sana kiroho. Hata ingawa maombi ni rahisi na hayafai kuonekana kama ambayo ni magumu, kuna pia nyakati ambazo maombi maombi ni kazi. Wakati mwingine lazima tujibidiishe katika maombi hadi jambo maalum ambalo Mungu ameweka katika mioyo yetu liondolewe au itabidi tungoje kwa subira au tujitolee kutoa kufanya kitu ili tusikie sauti ya Mungu. Lakini, wakati huo huo, tusiruhusu Shetani kutufanya tuamini kwamba lazima maombi yawe kazi ngumu na tata.

Shetani hufanya kazi usiku na mchana akijaribu kutuibia heshima ya kuwasiliana na Mungu. Hataki tushirikiane na Mungu kimawazo na bilaa shaka hataki tusikie sauti ya Mungu. Ninakuhimiza kujibidiisha na kuwa mwaminifu kwa kuwasiliana na Mungu na kugundua tena manufaa rahisi ya ushirika na Mungu ulio na utajiri, wenye ukamilisho, na unaotuza  ambamo wewe huzungumza naye, naye akazungumza nawe.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:  

Shiriki naye daima!

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon