Maombi Huzaa Utulivu

Maombi Huzaa Utulivu

Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. [Nitarahisisha, kutuliza na kuburudisha nafsi zenu]. —MATHAYO 11:28

Iwapo hatuna utuIivu, kwa kweli hatuamini, kwa sababu tunda la kuamini ni utulivu.

Kwa miaka mingi ya maisha yangu, ningedai, “Oh, ninamwamini Mungu; ninamtumainia Mungu.” Lakini sikuwa ninafanya mojawapo ya vitu hivyo, kwa sababu nilikuwa na fadhaa, wasiwasi, kisirani na mwenye kukasirika kila wakati.

Kama tu vile tunavyoweza kujihusisha katika shughuli za nje, tunaweza kujihusisha na shughuli za ndani. Mungu anataka tuingie sio tu kwa utulivu wake katika miili yetu, anataka pia tuingie katika utulivu wake katika mioyo yetu.

Kwangu mimi, kupata utulivu, faraja, raha, burudiko, pumziko, na kitulizo kilichobarikiwa kwa moyo wangu kinamaanisha kupata uhuru kutokana na shughuli mbaya za kiakili. Ina maana kukosa kuishi katika mateso ya kujiwazia, kila wakati nikijaribu kuzua jibu nisilokuwa nalo. Sina lazima ya kufadhaika; badala yake, ninaweza kubaki mahali pa amani tulivu na kutulia kupitia kwa maombi.

Ikiwa kwa kweli tunamwamini na kumtumainia Mungu, tumeingia katika utulivu wake. Tumeomba na kumtwika fadhaa zetu na sasa tunaishi katika amani timilifu ya uwepo wake wa kila siku.

Unaweza kuzungumza Neno lake kwa nia yako iliyofadhaika vile tu Yesu alivyoinenea dhoruba kwa kusema, “Amani, tulia.”

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon