Jinsi Ya Kuomba Maombi Ya Kuleta Matokeo

Jinsi ya Kuomba Maombi ya Kuleta Matokeo

Mkiniomba neno lolote kwa jina langu, nitalifanya. —Yohana 14:14

Nilifika mahali katika maisha yangu ya maombi ambapo nilisikitika, kwa hivyo nikaanza kumtafuta Mungu kuhusu jambo hilo. Nilitaka hakikisho kwamba maombi yangu yangeleta matokeo. Nilitaka kuwa na hakikisho kwamba nikiomba, nguvu zingeachiliwa katika hali niliyoomba kuhusu. Nilitaka vitu hivyo lakini kusema ukweli, sikuwa na hakikisho wala tumaini.

Bila shaka shetani hutaka kuiba tumaini letu kuhusu maombi. Watu wengi hueleza masikitiko kama yale nilikuwa nayo. Wanaomba lakini wakati huo wote wanashangaa iwapo wanasikika. Ni nini kibaya? Ninaamini kuwa huwa tunafikiria kimakosa kwamba tunahitaji kuwa watimilifu ili tuwe na nguvu katika maombi, lakini sivyo. Ndiyo maana tumepewa jina la Yesu kulitumia katika maombi!

Tunapoomba katika jina la Yesu, tunawasilisha kwa Mungu Baba, yote Yesu alio, wala sio tulio. Ninashukuru kwamba siombi kwa jina la Joyce; iwapo ningekuwa naomba hivyo, nisingekamilisha lolote! Roho Mtakatifu hutusaidia kuomba tunavyostahili, na jina la Yesu hutuhakikishia jibu! Kuwa mkakamavu katika maombi kwa sababu unalo jina lipitalo kila jina na kila ulimi unapolikiri, kila goti hupigwa (Wafilipi 2:10).


Omba kwa ujasiri, ukitarajia matokeo!

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon