Kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa. MATHAYO 7:8
Siku moja niliamka kichwa kikiniuma. Nilitembea nikiwa na maumivu ya kichwa karibu siku yote, nikimwambia kila mtu niliyekutana naye kuhusu vile nilisikia vibaya—hadi nilipogundua kuwa nilikuwa nimelalamika siku yote na sikuwa nimechukua wakati wa kuomba Mungu aondoe maumivu niliyokuwa nayo.
Kwa bahati mbaya, kwa baadhi yetu tabia hiyo ni ya kawaida. Sisi hulalamika kuhusu shida zetu na kutumia muda wetu mwingi tukijaribu kufikiri tutakachofanya ili kuzisuluhisha. Kila mara huwa tunafanya kila kitu isipokuwa kile kitu kimoja ambacho tunaambiwa kufanya katika Neno la Mungu: kuomba, ili tuweze kupokea na furaha yetu iwe timilifu (tazama Yohana 16:24).
Shukuru kuwa Mungu anataka kutimiza kila hitaji letu. Tuna haki ya ajabu ya “kuomba na kupokea,” na tunafaa kuomba kila wakati kama kimbilio la kwanza kwa kila hali.
Sala ya Shukrani
Ninakushukuru, Mungu, katika kila jambo, hata bila kujali hali ilivyo. Ninatamani kuwa mtu mwenye kushukuru sana kadri niwezavyo, na ninakuomba kunisaidia kufikia lengo langu.