Mazingira ya Ibada

Mazingira ya Ibada

Mpeni Bwana utukufu wa jina lake; mwabuduni Bwana kwa uzuri wa utakatifu. —ZABURI 29:2

Tunapomwabudu Mungu, tunamtambua kwa jinsi alivyo, yote ambayo ametenda katika maisha yetu, na yote ambayo atafanya bado.

Ibada sio kwa ajili yetu— ni kwa ajili ya Mungu. Lakini hata kama ibada sio kwa ajili yako, ibada hukubadilisha. Kwa kuanza kumwabudu Mungu kwa sababu ya mabadiliko ambayo tayari anafanya ndani yako, unapata kwamba mabadiliko hayo yanaanza kudhihirika zaidi na zaidi, na unaanza kuwa na viwango vipya vya utukufu wa Bwana. Kwa maneno mengine, Mungu yuko karibu na aabudiye, na atawamwagia wema wake wanaochagua kumwinua.

Kuna kuachiliwa kunakokuja kupitia kwa ibada. Wakati mwingine tunahitaji kuachiliwa kihisia au kiakili. Tunapomwabudu Mungu, tunaachilia mzigo wetu wa kiakili au kihisia ambao unaturudisha nyuma. Unamezwa katika wema na utukufu wa Mungu.

Ninawahimiza kuanza kuabudu asubuhi mapema. Abudu unapojitayarisha kuanza siku yako, na unapokuwa kazini au nje ukifanya shughuli zako. Na uabudu Mungu siku inapoisha kwa yote ambayo amekutendea. Utashangaa vile mambo yataanza kubadilika nyumbani na kazini ukimpa Mungu nafasi ya kwanza katika maisha yako.


Ibada hubuni mazingira ambapo Mungu anaweza kufanya kazi.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon